Msanii wa muziki mkongwe amabaye alifanya vizuri na nyimbo mbalimbali Inspekta Haroun amewashauri wasanii hususan wale wanaochipukia kutumia vizuri pesa zao na vilevile kuwekeza katika miradi tofauti nje ya muziki.
Inspekta a.k.a Babu akiongea na eatv amesema kuwa, kama msanii ni vizuri zaidi kuwa mjasiriamali pia kutokana na kuongeza kipato na kuwa na vyanzo vingi vya mapato ikiwa ni njia ya kuwaepusha na msongo wa mawazo.